Wanaharakati wa kulinda mazingira ya baharini wameeleza wasiwasi kuwa huenda mazingira  baharini yakaharibika zaidi kutokana na ukataji wa mikoko unaoendelea mjini Kilifi.

Wamesema kuwa kwa siku za hivi karibuni mikoko hiyo imekuwa ikikatwa na watu ambao baadaye huuza mikoko hiyo katika sehemu zengine za nchi hii.

Kiongozi wa wanaharakati hao Kassim Shali amesema kuwa kuna haja ya uchunguzi kamili kufanywa ili kufahamu ni akina nani wanaotekeleza uovu huo.

Maeneo ambayo mazingira hayo yameharibiwa zaidi ni katika fuo ya bahari ya Old Ferry,Uyombo,Watamu miongoni mwa maeneo mengine.

Wakati huohuo waziri wa mazingira kaunti ya Kilifi Kiringi Mwachitu amesema kuwa uchunguzi kuhusu uharibifu huo unaendelea ili kukabiliana na tatizo hilo.