Mwenyekiti wa muungano wa waathirika wa saratani nchini Prisca Wanjiru ametoa wito kwa serikali kuweka juhudi zaidi ya kuwapunguzia gharama za matibabu wakenya wengi ambao wanaugua ungojwa wa saratani ya matiti.

Prisca Wanjiru amesema kuwa licha ya huduma za bima ya afya ya kitaifa kuwa na nafuu kwa wagonjwa wa saratani matibabu ya ugonjwa huo yangali juu kwa wakenya hasa wale wenye mapato ya chini.

Wanjiru amesisitiza haja ya wanawake kufanya uchunguzi ili kubaini uwepo wa ugonjwa huo mapema.

Ameongeza kuwa ni muhimu kila mwanamke kuchunguza mwili wake mwenyewe kila mara na kumuona daktari iwapo kuna dalili zozote.

Wakati huo huo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza katika vituo mbali mbali vya afya vinavyotoa huduma za bure za uchunguzi wa saratani ya titi mwezi huu wa Oktoba.