Msimamizi wa watu wenye ulemavu kaunti ya TaitaTaveta Fatuma Kadzo amesema kuwa kwa sasa serikali ya kitaifa imeanza kubadilisha kadi za watu wenye ulemavu na kupewa kadi mpya zenye sajili kama vitambulisho vya kitaifa.

Akizungumza huko Werugha kaunti ndogo ya Wundanyi Kadzo amesema kuwa kadi za sasa zimekuwa zikitumiwa na walaghai, kwa maswla yao wenyewe.

Fatuma aidha ameongeza kuwa kadi hizo mpya sasa zitakuwa na nambari maalumu kama vile ya vitambulisho vya kitafa na kufunga mianya ya walaghai wanao zitumia kwa njia isiyo faa.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kaunti ya Taita Taveta kuhakikisha wanasaidia watoto wenye ulemavu nyanjani ili kuhakikisha wanapata msaada hitajika.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo