Wito umetolewa kwa wakaazi wa gatuzi dogo la Msambweni kaunti ya Kwale kuhakikisha wanafuata maagizo ya wizara ya afya dhidi ya kukabiliana na maambukizi ya covid-19.

 Akitoa wito huo naibu kamishina kaunti ndogo ya Wundanyi Victor Kisachi amesema kumeshuhudiwa ukame katika  sehemu nyingi za kaunti hiyo ila kwa sasa  mvua inanyesha na kuongeza kuwa sehemu za milimani hushuhudia maporoko ya ardhi.

 Aidha Kisachi amesema kuwa kwa sasa serikali inachukua tahadhari mapema ili kuzuia maafa kwa kuhakikisha wakaazi wanafahamishwa mapema kuepuka maafa hayo.