Ni sharti kwa vijana kupewa nafasi za uongozi ili kweza kuitumikia jamii.

Hii ni kauli yake Muwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Likoni Duncan Omuko maarufu kwa jina Kogalo.

Akizungumza huko Likoni kwenye hafla ya kuidhinishwa kuwania wadhifa huo na wazee wa jamii ya wajaluo, Omuko amesema wakati umefika ambapo vijana katika eneo bunge hilo la Likoni vilevile wanafaa kupewa nafasi za uongozi sawia na watu wengine katika jamii.

Omuko amesema kuwa eneo bunge la Likoni limesalia nyuma kimaendeleo kutokana na uongozi mbaya na kwamba ipo haja ya uongozi wa eneo hilo kubadilishwa.

Wakati uo huo, mwenyekiti wa jamii wa wajaluo Daniel Auwor amelaumu uongozi wa awali wa Likoni na kwamba umefeli na kwamba ipo haja ya wakaazi wa Likoni kupata uongozi bora kwa ajili ya maendeleo.

Mwandishi:Ibrahim Mudibo