Wizara ya afya imethibitisha visa vipya 170 vya Covid-19 na kufanya idadi ya maambukizi kuwa 320,399.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kiwango chanya cha maambukizi ni asilimia 4.7.

Idadi ya waliofariki nchini imeongezeka hadi 5,558 baada ya wagonjwa wengine wanne kufariki.

Kagwe amesema hivi sasa kuna wagonjwa 721 waliolazwa katika vituo mbalimbali vya afya nchini, huku 5,733 wapo chini ya mpango wa kujiuguza nyumbani.

Wagonjwa 40 wapo katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), 38 kati yao wakipata msaada wa kupumua huku wawili wakiwa na oksijeni ya ziada.

Wakati huo huo, wagonjwa 556 wamepona ugonjwa huo.Kufikia leo, jumla ya chanjo 11,553,637 zimetolewa kote nchini.