Serikali imetakiwa kulipa uzito swala la usalama wa majaji na wafanyikazi katika idara ya mahakama.

Akiongea na meza yetu ya Habari wakili wa mahakama ya juu mjini Kilifi carolyne chilango amesema inasikitisha kuona visa vya mashambulizi kwa wafanyikazi wa mahakama vikikithiri na hata kusababisha maafa kwa wengine.

Kauli ya wakili chilango ambae pia ni mwaniaji kiti cha useneta kauti ya Kilifi, inajiri siku mbili tu baada ya gari alilokua akisafiria jaji wa mahakama ya garsen na wafanyikazi wenzake kushambuliwa kwa risasi na watu wasojulikana katika barabara ya lamu.

Wakili huyo ameonya endapo visa hivyo vitakithiri basi huenda vika athiri utoaji huduma za haki na usawa mahakamani.

 


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani