Huku uchaguzi mkuu wa Agosti 9 ukiwadia, wawaniaji wa nyadhfa mbalimbali za uongozi wanawashinikiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuwachagua viongozi wenye sera za maendeleo.

Mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wadi ya Bofu eneo bunge la Likoni Chaka Juma amesema ukosefu wa maendeleo katika jamii kumesababishwa na wakaazi kuwachagua viongozi kwa misingi isiyofaa.

Ametaja kuwa wadi hiyo imetengwa katika masuala ya maendeleo, elimu na afya kutokana na viongozi waliyotangulia kuwa wabinafsi na wasiyojali maslahi ya wakaazi.

Aidha Chaka ambae amekuwa mwalimu kwa muda mrefu, amesema iwapo atachaguliwa kuiwakilisha wadi hiyo, atahakikisha kuwa amezitimiza ajenda zake kwa manufaa ya wakaazi wa eneo hilo akiwasisitiza wakaazi wa wadi hiyo, eneo bunge la Likoni na Mombasa kwa jumla kutopiga kura kiwa mirengo ya kikabila.

Mwandishi:Ibrahim Juma Mudibo