China imeripoti wagonjwa wapya 393 walioambukizwa virusi vya korona, ingawa hakukuwa na mgonjwa yeyote aliyefariki kwa ugonjwa wa UVIKO-19 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Idadi ya wanaogundulika kuwa na maambukizo hayo bila kuonesha ishara yoyote ni kubwa zaidi ya wale wenye ishara.

Kufikia jana Jumapili, China bara ilikuwa imeshathibitisha maambukizo 229,594 ya wagonjwa wenye dalili za maambukizo, huku idadi ya wasiokuwa na dalili ikipindukia mara tatu ya hiyo.

Kuendelea kuwapo kwa maambukizo mapya ya virusi hivyo nchini China, taifa vilikoanzia na lililokuwa limefanikiwa kuvidhibiti, kunatajwa kuzusha wasiwasi wa kurejea upya kwa wimbi jengine la ugonjwa huo.