Watu wanne wakiwemo polisi wawili wameuawa na waasi wenye silaha huko Maidan kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Shambulio hilo lilimlenga Mbunge Malik Liaqat Khan aliyejeruhiwa na ambaye ni kutoka chama cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Imran Khan.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo lililoendeshwa katika mkoa wa kihafidhina wa Khyber Pakhtunkhwa, unaotawaliwa na chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf.

Eneo hilo limekuwa ngome ya kiongozi mkuu wa kidini marehemu Sufi Mohammad, ambaye alikuwa na msimamo mkali wa Uislamu katika miaka ya 1990 na baadaye aliwaongoza wafuasi wake katika mapigano nchini Afghanistan dhidi ya vikosi vya Marekani na washirika wake.