Maafisa wa Ukraine wamesema leo kuwa wanajeshi wa Urusi wameuripua mji wa kaskazini wa Chernihiv licha ya ahadi za awali za Moscow kuwa inapunguza pakubwa baadhi ya shughuli zake za kijeshi nchini Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hakuna sababu ya kuliamini tangazo la Urusi kuwa itapunguza shughuli za kijeshi karibu na mji mkuu Kyiv, pamoja na mji wa kaskazini wa Chernihiv, ukizingatia kinachoendelea katika maeneo hayo.

Mazungumzo ya jana mjini Istanbul yalitoa matumaini ya kumaliza vita hivyo ambavyo vimewauwa maelfu ya watu na kusababisha Waukraine milioni nne kuikimbia nchi.

Mazungumzo hayo yalitarajiwa kuendelea leo lakini pande mbili za mzozo huo ziliamua kurejea makwao kwa ajili ya mashauriano zaidi.

Kwa hisani ya Dw swahili.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani