Ujerumani imesema inawafukuza wanadiplomasia 40 wa Urusi kama jibu kwa mauaji ambayo wanajeshi wa Urusi wanatuhumiwa kuyafanya katika wa Bucha nchini Ukraine.

Ufaransa na Lithuania pia zimesema zitawafungisha virago wanadiplomasia wa Urusi, hatua ambazo Urusi imesema itazijibu.

Mshauri wa rais wa Marekani kuhusu masuala ya usalama wa taifa, Jake Sullivan amesema rais Joe Biden atashirikiana na nchi washirika kuhakikisha kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin anawajibishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu au kwingineko.

Ukraine imeituhumu Urusi kufanya mauaji ya halaiki katika mji wa Bucha, ambako vyombo vya habari vya Ukraine vimesema kumegunduliwa maiti 340 hadi sasa.

Urusi imezikanusha tuhuma hizo, ikisema taarifa hizo ni za kutunga kwa lengo la kuichafua.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani