Serikali kupitia wizara ya mawasiliano na teknolojia nchini Imezindua mpango mkuu wa kitaifa wa kidijitali wa mwaka 2022-2030 kuelekeza nchi mbele kuhusu uwekezaji wa mawasiliano na teknolojia kwa lengo la kuharakisha mageuzi ya kidijitali.

Akizundua mpango huo Waziri katika wizara hio Joe Mucheru amesema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuimasrisha sekta ya teknolojia na mawasiliano nchini.

Mpango huu umebainisha miradi mikuu 19, ambayo serikali itazingatia, ili kuharakisha mageuzi ya kidijitali nchini.

Baadhi ya yanayolengwa kutekelezwa katika mpango huo ni usambazaji wa huduma za mtandao katika shule elfu 40 pamoja na taasisi za kiserikali na kupeana mafunzo ya teknolojia kwa vijana.

Mucheru ameyasema haya baada ya kufungua rasmi kongamano lilojumuisha washikadau kutoka sekta ya mawasilaino na teknolojia hapa nchini na Africa kwa jumla.

Mucheru amepigia upatu ushirikiano kati ya washikadau sekta hio huku akiweka wazi kwamba teknolojia ina jukumu kubwa katika maendeleo.

 

 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani