Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.
Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi wa baharini katika baraza la magavana, amesema hiyo ndio njia pekee itakayozuia wavuvi kutoka mataifa ya nje kunufaika na bahari ya humu nchini.
Ameeleza kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuwekwa ili kutumia kikamilifu raslimali zote zilizo baharini.
Ametolea mfano jinsi mataifa yaliyoendelea yanatumia fursa ya bahari kuvuna mafuta na gesi, kawi ya kutumia mawimbi, uvunaji wa hewa kaa pamoja na usafiri wa baharini.
Kauli ya Timamy inajiri huku jumuiya IGAD ikitoa wito kwa mataifa ya bara Afrika kuwekeza zaidi katika uchumi samawati ili kuchangia katika mapato ya mataifa yao.Katibu mkuu wa IGAD Dr Workneh Gebeyehu ameeleza kuwa sekta ya uchumi wa baharini ni muhimu kwa bara Afrika na huenda ikawa moja wapo ya sekta zitakazochangia kwa kiasi kikubwa mapato na ukuwaji wa uchumi.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo