Jumla ya mahafala 124 wamefuzu kwenye hafla ya chuo cha ya utabibu cha North coast medical training college kaunti ya Kilifi .

Hafla hiyo iliyoandaliwa Ijumaa ya tarehe 23 juni mwaka huu ilihudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka eneo la pwani.

Akiongea na wanahabari mkurugenzi wa North Coast medical training college Ruben Waswa amesema chuo hicho huandaa hafla ya kufuzu kwa mahafala mara mbili ili kuhakikisha wanafunzi hawakai sana kusubiri kufuzu ilia pate cheti chake mapema.

Mkurugenzi huo aidha amepongeza ushirikiano uliopo kati ya chuo hicho na jamii iliyopo karibu na chuo hicho.

Ameongeza kuwa chuo hicho kimeboresha biashara zilizopo karibu na chuo hicho huku pia baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanatoka maeneo karibu na chuo hicho

Kulingana na mama mtaa wa eneo la Bomani huko Kikambala kaunti ya Kilifi, Janet Karisa amesema tangu kuazinshwa kwa chuo hicho vijana wengi wamepata nafasi za ajira katika chuo hicho.

Aidha ameeleza kuwa chuo hicho kimesaidia jamii ya eneo la Bomani kuhusu masuala ya afya pamoja na kutoa msaada wa viti vya magurudumu kwa wenye ulemavu wa kutotembea.

Ameongeza kuwa chuo hicho kimefungua hospitali inayoshughulikia kina mama wajawazito katika eneo hilo.