Serikali ya kaunti ya mombasa kupitia wizara yake ya elimu imejitolea kuwapa nauli ya shilingi 150 kwa wanafunzi ili kuhudhuria mpango wa ushauri na nasaha uliozinduliwa na serikali ya kaunti hiyo wakati huu wa likizo.

Zaidi ya wanafunzi elfu 8 wa shule za upili kaunti ya Mombasa wamenufaika na mpango huo wa ushauri na nasaha yaani mentorshipo programe.

Mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha wanafunzi kupata ushauri nasaha wakati huu wa likizo, mafunzo ili kuwaepusha kujiingiza katika tabia potofu.

Akizungumza alipozuru shule mbalimbali hapa Mombasa kutathmini maendeleo ya mpango huo gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewataka wanafunzi kutia bidii ili kuboresha Zaidi kiwango cha elimu Mombasa.

Licha ya wengi wao kutoka katika jamii maskini serikali ya kaunti kupitia wizara ya elimu kaunti ya Mombasa inawapa shilingi 150 ya nauli ya kila siku huku wakiwekewa shilingi 250 kila siku kama mjazo wa basari ili kupiga jeki juhudi za wazazi wao.

Kwa upande wake waziri wa elimu kaunti ya Mombasa Daktari Mbwarali Kame amesema mpango huo umepunguza visa vya wanafunzi kujihusisha na tabia potofu wakati wa likizo.

Hata hivyo ana imani kuwa kiwango cha elimu Mombasa kitaimarika zaidi.