Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema serikali yake imewekeza zaidi katika sekta ya afya ili wananchi mashinani wapate huduma bora za afya.

Gavana huyo ameongeza kuwa wanapania kuongeza maafisa zaidi wa afya katika vituo mbalimbali vya afya kwenye kaunti hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa kuna dawa za kutosha na vifaa vya kisasa vya matibabu.

Achani ameyaongea haya kwenye ufunguzi wa zanahati ya Mwakijembe katika wadi ya Ndavaya eneo bunge la Kinango,huku idadi ya zahanati ikifikia 165 katika maeneo mbalimbali kaunti hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wakaazi wa eneo la Mwakijembe wakiongozwa na Menza Rocha wamepongeza ujenzi wa zahanati hiyo wakisema itawapunguzia mwendo hususan kwa mama wajawazito waliokua wakilazimika kutembea mwendo mrefu wa zaidi ya saa mbili kutafuta huduma za matibabu.

 


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani