Serikali ya kaunti ya Mombasa imefunga baadhi ya vituo vya Gesi vinavyoendeleza biashara kinyume cha sheria.

Hii ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya vituo vya gesi hapa Mombasa vinaendelea na biashara bila ya vibali.

Akizungumza alipozuru baadhi ya vituo kuthatmini uendelezaji wa biashara hio, gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameamuru kufungwa kwa vituo hivyo akisema kuwa vinahatarisha maisha ya wakaazi.

Hatua ya gavana Nassir inajiri kufuatia tukio la hivi majuzi huko Jijini Nairobi eneo la Embakasi ambapo kituo kimoja cha gesi kililipuka na kupelekea mauaji ya watu 7 huku watu 280 wakipata majeraha.

Nassir sasa ameziomba kampuni kubwa zinazo sambaza gesi hapa Mombasa kusitisha zoezi hilo kwa vituo ambavyo havijaidhinishwa rasmi na serikali ya kaunti, mamlaka ya kuthibiti Mazingira NEMA Pamoja na shirika la kudhibiti kawi nchini EPRA.

Baadhi ya maeneo ambayo tayari baadhi ya vituo vya gesi vimefungwa ni Majengo, Ganjoni, Tudor na Kongowea.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo