Idadi ya visa vya Covid-19 nchini vimefika 161,393 baada ya watu wengine zaidi 489 kupatikana na virusi hivyo.

Visa vipya vinatokana na  sampuli ya vipimo 4,426 vilivyofanywa kwa saa 24, ikiwakilisha kiwango cha chanya cha asilimia 11.

Visa vipya vinajumuisha Wakenya 449 na wageni 40 wenye umri kati ya miezi minne na miaka 102.

Katibu msaidizi wa utawala katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amethibitisha kuwa vifo 20 zaidi vilirekodiwa kufikisha idadi jumla ya vifo 2,825.

Kumi na moja ya vifo viliripotiwa tarehe tofauti wakati tisa vimeripotiwa ndani ya saa 24 kutika kwa vituo vya afya.

Wagonjwa wengine 1,164 kwa sasa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya wakati 6, 603 wako katika mpango wa huduma ya nyumbani.

Wagonjwa 153 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi ICU, 28 kati yao wako kwenye msaada wa upumuaji, 99 juu ya oksijeni ya ziada na wengine 26 chini ya uchunguzi.

Wagonjwa wengine 119 wako kando na oksijeni ya ziada kati yao 111 wako katika wodi za jumla na wanane katika kitengo cha utegemezi.

Aman amethibitisha kuwa wagonjwa wengine 552 walipona kutoka kwa virusi, 303 kutoka vituo vya afya kote nchini na 249 kutoka kwa mpango wa huduma ya nyumbani.

Kwa upande wa chanjo, Wakenya 900, 459 hadi sasa wamechanjwa, 524, 720 maafisa wa umma wakiwemo wale walio na umri wa zaidi ya miaka 58, Ambapo 159,308 ni wahudumu wa afya, 140,354 ni walimu na 76, 077 ni wa usalama.