Ruth Keah ndiye mwanahabari bora wa Radio mwaka wa 2021 nchini.

Ruth ambaye ni mhariri mkuu katika idhaa ya Radio Rahma alituzwa kwenye hafla ya kila mwaka ya kuwazawadi wanahabari waliofanya vyema katika utendakazi wao.

Baadhi ya vitengo ambavyo ameshiriki ni pamoja na maendeleo,mazingira,Teknolojia na mawasiliano,podcast na hatimaye kutuzwa kama mwanahabari bora wa radio mwaka wa 2021.

Miongoni mwa waliofanya vyema na kuwa miongoni mwa watatu bora katika vitengo mbalimbali katika mashindano hayo ni mkuu wa vipindi katika idhaa ya Radio Rahma Faiz Musa Abdhallah.

Ambapo alitambuliwa katika kitengo cha Biashara, Maendeleo,uongozi bora,na Teknolojia na mawasiliano.

Wanahabari mbalimbali kutoka vitengo vya Televisheni na Magazeti pia wametunikiwa tuzo mbalimbali.

Jumla ya Makala 1,119 yalitumwa kwenye mashindano hayo mwaka huu.

Sherehe hizo hufanywa kila mwaka kama kilele cha kusherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni ambayo huadhimishwa tarehe 3 Mei kila mwaka.

Sherehe hizo zimeandaliwa na baraza la vyombo vya habari nchini jijini Nairobi ,ambapo mgeni wa heshima mwaka huu amekuwa kaimu jaji mkuu nchini Philomena Mwilu.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo