Huku suala la ajira litajwa kuwa donda sugu linalowasumbua vijana hapa Mombasa,mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kuendeleza mradi wa mafunzo ya skills mitaani kwa vijana wote wa kaunti ya Mombasa.

Mradi huo ambao kwa sasa umewafaidi zaidi ya vijana elfu 11 wa eneo bunge la Mvita kujipatia ujuzi wa kazi za mikono Nassir amesema mradi huo sasa utapanua mbawa zake na kuuendeleza ili kuwafaidi vijana wote wa kaunti ya Mombasa.

Akizungumza huko Likoni wakati akiendeleza kampeni za kujipigia debe kurithi kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Nassir vile vile amesema atafufua biashara kwa vijana na akina mama wote kutoka maeneo mbali mbali kaunti ya Mombasa.