Wazee wa baraza la Kaya kutoka jamii ya Mijikenda wamewataka wanasiasa kufanya siasa zao kwa amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi wa Agozti 9.

Wakizungumza katika kaunti ya Mombasa wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa baraza hilo kanda ya Pwani Shaaban Ndegwa amekemea vikali vujo zinazodhihirika kwenye mikutano mbalimbali ya kisiasa na kutaka hali hiyo kukomeshwa mara maoja.

Ndegwa amesema kwamba kila mwaniaji wa wadhfa wowote kwenye uchaguzi ujao anayo nafasi na haki ya kuuza sera zake kwa wananchi mahali popote kwa amani bila fujo.

Aidha mzee huyo wa Kya amewaonya wanasiasa dhidi ya ya kuwatumia vijana kuzua vurugu kwenye mikutano ya wapinzani wao vilevile akiwataka vijana kuepuka wanasiasa wenye tabia hizo.

Kauli ya Ndegwa imeungwa mkono na Mwanamwenga Chigamba Nyanje akiwasisitiza wakenya kuepuka siasa za kikabila na kuiga mfano wa taifa la Tanzania.

Kwa upande wao Luvuno Gari pamoja na Mwaka Dzombo wametaka wanasiasa kuzingatia amani huku wakihofia masomo ya watahiniwa kusambaratika endapo vurugu zitatokea pamoja hali za kina mama na watoto kuathirika.

 Mwandishi:Ibrahim Mudibo