Wito umetolewa kwa wakaazi hapa Mombasa kukumbatia utangamano,uwiano na kutupilia mbali masuala ya ukabila msimu huu ambapo kampeni za uchaguzi zimeshamiri.

Wito huo umetolewa na Mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir.

Nassir amesisitiza haja ya wakaazi hapa Mombasa na Pwani kwa ujumla kuunda udugu,umoja ,uwiano na utangamano ili kuepuka vurugu zinazo shuhudiwa ifikipo wakati wa uchaguzi.

Nassir ametaja masuala hayo kama njia bora ya kuunda maadili mema kwa vizazi vijavyo.

Nassir amewahimiza wakaazi kuendeleza undugu na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za ukusanyaji damu zinazoendeshwa na mashirika mbalimbali ili kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji bidhaa hio adimu hospitalini.