Mgombea wa uwakilishi wa kike Kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya Chama cha United Green Movement Hamisa Maalim Zaja amesema endapo atachaguliwa kama mwakilishi wa kike katika kaunti ya Mombasa, atashirikiana na wafadhili mbalimbali kufanikisha miradi mingi ya kijamii.

Zaja ametaja kuwa yuko katika nafasi bora zaidi ya kuimarisha maisha ya Wakaazi wa Mombasa.

Wakati uo huo, Kiongozi huyo anayewania uwakilishi wa kike wa Kaunti ya Mombasa kwa mara ya pili sasa ameitaja sekta ya afya kama moja wapo ya vipengele muhimu atakavyojizatiti kuhakikisha kwamba vimeboreshwa kwa kushirikiana na wafadhili.