Rais Uhuru Kenyatta amemkashifu Naibu wake William Ruto kwa kuilaumu serikali mara kwa mara ambayo anafanyia kazi, akisema ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakenya.

Rais amesema naibu wake amekuwa akiishtumu serikali na kuwapa wakenya ahadi za uongo kwa kile anachonuia kuwafanyia wakenya atakaposhinda urais kwenye uchaguzi wa agosti 9 .

Akizungumza siku ya Jumamosi alipoongoza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika mwaka huu hapa nchini nchini katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano huko Nairobi, Rais Kenyatta ameelezea masikitiko yake kutokana na matamshi ya Naibu wake akisema ameshindwa kutekeleza majukumu yake wakati anafanyia serikali.


Ruto amekuwa akikosoa utendakazi wa utawala wa Jubilee ambao amekuwa sehemu yake baada ya kuachana na Rais Kenyatta.
Rais amewataka wakenya kutowchagua viongozi ambao walikuwa serikalini na kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Hatahivyo rais Kenyatta amemtetea waziri wa kilimo Peter Munya kutokana na mabadiliko aliyoyafanya katika sekta ya kilimo akisema wengine walishindwa kutekeleza majukumu yake alipokuwa akihudumu katika sekta hiyo.