Mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amekemea vikali tukio la hapo jana ambapo watu wasiojulikana walirusha kitoa machozi kwenye mkutano wa hadhara ambao mgombea mwenza wa kinara wa Azimio la umoja-One kenya Martha Karua na Mama Idda Odinga walikuwa wakihutubia umma kaunti ya Kisii.

Akizungumza hapa Mombasa, Nassir amewashtumu viongozi wa muungano wa upinzani kwa kile anachokisema kuwa ni njama yao ya kutaka kuharibu mikutano ya Karua baada ya kuona kuwa anapata ufuasi mkubwa wa watu.

Aidha Nassir sasa anawaomba viongozi wa kisiasa nchini kuepuka siasa za vurugu kwa sababu ya tamaa zao binafsi ili kuepusha kushuhudiwa kwa matukio ya umwagikaji damu kama ilivyoshuhudiwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Haya yanajiri huku zikiwa zimesalia siku 38 pekee kufikia uchaguzi mkuu nchini.