Mwaniaji wa ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya ODM Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kuendeleza miradi iliyosalia kaunti ya Mombasa.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Jitoni eneo bunge la Jomvu, Nassir amesema yuko tayari kukamilisha barabara zilizo salia ikiwemo barabara hiyo inayounganisha Jitoni na Jomvu kuu.

Nassir ambaye alikuwa ameandamana na mbunge wa eneo hilo Badi Twalib Badi amewakemea vikali viongozi wa kisiasa wanaondeleza siasa za kejeli na kuwataka kuwahudumia wakaazi kimaendeleo.

Kwa upande wake mbunge wa Jomvu wa Jomvu Badi Twalib amesisitiza haja ya wakaazi kuchagua viongozi wao kwa mfumo wa 6 piece.

Vile vile amewataka wakaazi wa Mombasa kujiweka kando na viongozi wa kisiasa wanaogura vyama na kujiunga na vyengine akidai wanamaslahi yao binafsi.