Kamishena wa Kwale Gideon Oyagi amewaonya wanasiasa dhidi ya kununua vitambulisho vya kupigia kura kutoka kwa wananchi wakati huu wa uchaguzi.

Oyagi amesema kwamba wanasiasa watakaopatikana wakinunua vitambulisho hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kamishena huyo aidha amewashauri wakaazi wa kaunti hiyo kutouza vitambulisho vyao ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu wiki ijayo.

Kwa upande wao viongozi katika eneo hilo wametoa wito kwa wakenya kudumisha amani huku vijana wakitakiwa kutohadaiwa na wanasiasa kuuza kura zao.

Mgombea wa kiti cha useneta wa Kwale kupitia chama cha Safina Hezron Obadiah na mgombea wa kiti cha ubunge wa Matuga kwa tikiti ya chama cha Jubilee Hassan Chidzuga ni baadhi ya viongozi hao.