Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Juu Jumatatu linatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu ombi la kutulipilia mbali matokeo ya urais.

Kesi hiyo ililowasilishwa na Azimio la Umoja One mgombea urais wa Kenya Raila Odinga na walalamishi wengine sita.

Mahakama hiyo chini ya usimamizi wa Jaji Mkuu Martha Koome itatoa uamuzi wake kwa kuzingatia masuala tisa ambayo yaliibuliwa katika maombi jumuishi ya kupinga matokeo ya urais ya Agosti 9.