Mahakama ya Juu humu nchini leo itatoa uamuzi wake kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya Habari, mahakama hiyo imesema itatoa uamuzi huo mwendo wa saa sita mchana.

Majaji saba wa mahakama hiyo walianza kuandaa uamuzi huo siku ya Ijumaa baada ya kuhitimisha kusikilizwa kwa pingamizi iliowasilishwa kwa siku tatu.

Huku hayo yakijiri, huduma ya taifa ya polisi imetangaza kufungwa kwa barabara kadhaa Jijini Nairobi.

Katika taarifa kwa wanahabari, kamanda wa Traffiki katika eneo la Nairobi Vitalis Otieno, ameagiza kwamba barabara ya Ngong’ itafungwa katika eneo la Ngong Road 1st Avenue mkabala na Jumba la NHIF.

Hii inamaanisha kwamba waendeshaji magari hawataruhusiwa kuingia kati kati mwa Jiji kupitia barabara ya Kenyatta Avenue na Cathedral road, lakini badala yake watatumia barabara ya Haile Selassie Avenue.

Aidha, kamanda huyo wa Traffiki anasema barabara za Cathedral Road na Milimani Ngong Road zinazoelekea katika Mahakama za Milimani zitafungwa katika makutano ya barabara za Kenyatta Avenue na Valley Road, karibu na Jumba la NSSF.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo