Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema  itarudisha kwa serikali ardhi zote ambazo zimenyakuliwa na mabwenyenye katika kaunti hiyo.

Katika ziara yake ya kutathmini maswala ya raslimali za kaunti hiyo mjini Kilifi,gavana wa kaunti hiyo Gedeon Mungaro amewaonya wale wote ambao wamenyakua ardhi hizo kuwa watapokonywa na kurudishwa kwa serikali.

Kulingana na Mungaro,ardhi za umma zimenyakuliwa jambo ambalo limepelekea uhaba wa ardhi wa kujenga maofisi na taasisi zengine za kiserikali.

Amesema kuwa uchunguzi wa ardhi hizo utaanza hivi karibuni na kusema kuwa wanyakuzi wa ardhi hizo pia watachukuliwa hatua za kisheria.

Wakati huohuo gavana Mungaro amesema serikali ya Kilifi iko na mpango maalumu wa kujenga jengo kubwa ambalo litamiliki afisi za idara zote za serikali hiyo.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itapunguza gharama ya kifedha ambayo serikali hiyo inalipa kwa ofisi ambazo wamekodisha kwa wamiliki wa kibinafsi.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani