Baadhi ya wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Kwale sasa wanapendekeza nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa polisi ili kuboresha utendakazi wao.

Mwenyekiti wa wahudumu hao kaunti ya Kwale Nehemiah Kinywa amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kukabiliana na visa vya ufisadi katika sekta ya hiyo.

Kinywa ametaja malipo duni kuwa chanzo cha baadhi ya maafisa wa polisi kuchukua hongo kutoka kwa wahudumu wa bodaboda.

Kwa upande wake mwanaharakati wa kijamii kaunti hiyo Gabriel Barasa ameitaka serikali kuzidisha mpango wa kutoa ushauri nasaha kwa maafisa wa polisi ili kukabiliana na matatizo ya afya ya akili.

Barasa amesema kuwa visa vya mauaji ya polisi huchangiwa na ukosefu wa ushauri miongoni mwa maafisa wanaokumbwa na msongo wa mawazo.