Makundi ya matembezi kaunti ya Kwale na Kilifi kwa ushirikiano na shirika la watu wenye ulemavu wa kuona la African Union of the Blind limewahimiza madereva kuzingatia sheria za barabarani.

Mwakilishi wadi ya Mariakani kaunti ya Kilifi Martha Koki kutoka kundi la Mariakani Walk Movement, amewataka madereva kutilia maanani sheria hizo ili kuzuia ajali za barabara.

Kauli yake imeungwa mkono na afisa wa shirika la African Union of the Blind Abraham Mateta aliyetaka pia usalama wa watu wasioona kuzingatiwa hasa na watumizi wa barabara.

Kwa upande wao wanachama kutoka kundi la Diani Walkers na Kwale Walk Movement wamesema kuwa matembezi ni mazoezi muhimu kwa afya ya mwili.

Wakiongozwa na Hamza Abdallah, wanachama hao wametumia fursa hiyo kutoa hamasa kwa umma kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabara.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo