Shirika la NACADA limeweka wazi kuwa litatoa ripoti kamili ya uchunguzi kuhusu utumizi wa dawa ya kulevya inayokisiwa kuwa Fentanyl.

John Muteti kaimu mkurugenzi wa NACADA,amesema uchunguzi unaendelea na watatoa ripoti kamili baada ya siku 14 zijazo.

Haya yanajiri baada ya video kusamba mitandaoni ikionyesha vijana wanatumia mihadhrati hio ambayo wanakisia kuwa ni mchanganyiko wa dawa za kulevya.

Kwa upande wake Hussain Taib kutoka Mewa ameitaka idara ya usalama na vitengo vingine vya serikali na visivyo kvya kiserikali,kuungana katika kupiga kukabili ongezeko la utumizi wa mihadharati.