Serikali ya kaunti ya Kwale imelazimika kupeleka magari matatu ya kusambaza maji katika eneo bunge la Kinango kufuatia makali ya ukame eneo hilo.

Akizungumza huko Kwale Mvurya amebainisha kuwa zaidi ya wakaazi laki moja wanalengwa kufaidika na maji yatakayosambazwa na magari hayo huko Kinango.

Vilevile amedokeza kuwa wananendeleza mikakati na serikali kuu kupata msaada wa chakula kwa ajili ya wakaazi walioathirika na makali ya ukame.

Wakati huo huo huenda changamoto ya uhaba wa maji safi katika eneo bunge la Msambweni na Matuga huko Kwale ukapata suluhu baada ya benki ya dunia kufadhili mradi wa maji.

Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya akizungumza baada ya kutia sahihi mkataba na wakandarasi watatu waliopata zabuni ya kuteleza miradi huo amesema kuwa ni njia mojawapo kutatua tatizo la ukosefu wa maji kwa kukidhi mahitaji ya wananchi ili kudumisha usafi na kuboresha afya.

Mradi huo ikiwemo uchimbaji wa visima 11, usambazaji wa maji hayo vitongojini na ujenzi wa maabara ya kupimia maji kuhakikisha ni salama yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa mda wa mwaka mmoja na kugharimu shilingi bilioni 1.4.