Huduma za watoto wachanga katika kaunti ya Kilifi zitaimarika zaidi baada ya jengo maalum la watoto wachanga ambao hawajafikisha wakati wa kuzaliwa  almaarufu Njiti kufunguliwa rasmi.

Jengo hilo limefunguliwa katika hospitali kuu ya rufaa ya kaunti ya Kilifi ambalo lilijengwa kwa ushirikiano wa serikali ya kaunti hiyo na wakfu wa Safaricom.

Kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo hilo,gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi amesema kuwa jengo hilo liko na vifaa vya kisasa vya kuhudumia watoto hao jambo ambalo amebaini kuwa litapunguza vifo vya watoto ambao wanazaliwa kabla ya kufika wakati wa kuzaliwa.

Kulingana na Kingi jengo hilo limegharimu kima cha shilingi milioni hamsini na tatu ambapo serikali hilo ilitoa milioni thelathini na nane nao wakfu wa Safaricom ukatoa kima cha milioni kumi na tano.

Jengo hilo pia lina vitanda sitini pamoja na madaktari ambao wamehitimu vyema.

Naye mmoja wa wadhamini wa wakfu huo Rita Okuthe amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa miradi ya afya kwa jamii.

Rita ameleza kufurhishwa kwake na jinsi serikali ya kaunti hiyo ilivyoshirikiana na wakfu huo katika kufanikisha mradi huo.