Visa vya dhuluma za kijinsia kaunti ya Taita Taveta vimetajwa kuendelea kukithiri huku wanao dhulumiwa wakikosa haki.

 Akitoa kauli hiyo mshauri wa maswala ya jinsia katika ofisi ya gavana Piricilah Mwangeka ametaja mapenzi ya watu wa jinsia mojo,ugomvi nyumbani kama miongoni mwa dhuluma zinazoshuhudiwa kwa sasa.

 Mwangeka ameongeza kuwa mara nyingi sababau zinazo tolewa na wanaotekeleza dhuluma hizo hazina msingi na kusema kuwa ni wakati sasa kwa jamii kusimama pamoja ili kuhakikisha dhuluma hizo zanakomeshwa.

 Wakati huo huo Mwangeka amewaomba  viongozi wa kidini kutoa mwongozo katika jamii ili kuhakikisha kuwa wanafunzwa maadili mema.