Serikali imewahakikishia wakaazi wa kaunti ya Lamu kwamba itaimarisha zaidi oparesheni za kiusalama katika kaunti hiyo.

Katibu katika wizara ya usalama wa ndani daktari Karanja Kibicho amaesema kwamba hii ni baada ya eneo hilo kushuhudia mashambulizi ambayo hadi sasa hayajabainika wazi iwapo wanaohusika ni wanamgambo wa Al-shabab au magenge ya kihalifu.

Kibicho amesema Kaunti ya Lamu sasa imekuwa eneo la oparesheni kali za kiusalama ili hali hiyo idhibitiwe na shughuli mbalimbali za kiuchumi ziendelee kama kawaida.

Kibicho amesema vitengo vya usalama vinafanya kila juhudi ili kudhibiti hali hiyo tata ya uhalifu katika Kaunti hiyo.

Kauli ya Kibicho inajiri huku Kufikia sasa watu 12 wakiwemo maafisa 4 wa GSU wameuwawa katika uvamizi huo katika maeneo ya Mpeketoni na Hindi Kaunti hiyo ya Lamu.

Mwandishi:Ibrahim Mudibo


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo