Familia moja kutoka huko Changamwe hapa kaunti ya Mombasa inaomba msaada wa matibabu ya mtoto wao anayeugua saratani ya damu.

Familia hiyo ya Charles Sanga Chikanda inasema mtoto wao Daniel Mbura mwenye umri wa miaka 10 na mwananfunzi wa gredi ya 3 alianza kuugua ugonjwa huo Julai mwaka jana.

Kulingana na familia hiyo baada ya matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta mtoto huyo sasa anahitajika kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Kulingana na Abigael Mbura ambaye ni mama wa mtoto huyo matibabu hayo yatagharimu takriban 5.5 fedha za Kenya hali anayoitaja kuwa changamoto kwao.

Kwa sasa familia hiyo inawaomba wahisani kujitokeza ili waweze kuwasaidia kumudu gharama hizo.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo