Watu 368 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 319,379 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.1.

Vile vile watu 823 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 287,963, 707.Kuna wagonjwa 865 ambao wamelazwa hospitalini, 7,762 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 46 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,345,649.