Imebainika kuwa zaidi ya wagonjwa elfu 3 kaunti ya Taita Taveta wanatembelea kliniki ya matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu na wengine zaidi ya wagonjwa elfu 14 hutembelea kliniki ya matibabu ya ugonjwa wa sukuri.

Hii ni kwa mjibiu ya wizara ya afya kupitia waziri wa afya kaunti hio John Mwakima.

Kulingana na waziri huyo asilimia kubwa ya watu wazima kaunti ya Taita Taveta wanao ugua magonjwa hayo huenda wengi wao wamekosa, lishe bora wakiwa wachanga.

Aidha Waziri huyo amewataka wazazi kaunti ya Taita Taveta kuzingatia lishe bora kwa watoto wao wachanga ikitajwa kuwa njia moja wapo ya kuwakinga na magongwa ambayo huchangiwa na ukosefu wa lishe bora wakiwa wadogo, na hata baadae kwa maisha yao.

Mwakima ameongeza kuwa wizara yake itaendelea kutoa hamasa kwa wananchi hasa akina mama walio na Watoto wachanga juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa watoto