Idara ya utawala eneo la Tana Delta haitaruhusu wanasiasa kufanya kampeni zao katika maeneo ya shule wakati huu ambapo wanafunzi wanajitayarisha kwa mitihanai na hata watakapokuwa katika mitihani.

Naibu kamishna wa Tana Delta John Kipsiwa amesema tayari wamekubaliana na wakuu wa shule pamoja na wadau wengine wa elimu eneo hilo kuwa ni wanafunzi pamoja na wadau wengine wa elimu pekee ndio wataruhusiwa kufika maeneo ya shule wakati wa mitihani na wala sio wanasiasa.

Amesema hii ni kuwahakikishiawanafunzi mazingira mazuri ili waweze kufanya mitihani yao kwa utulivu akisema kuwa kuruhusu watu kuingia maeneo ya shule kiholela huenda kukahujumu kanuni za mitihani.

Aidha amewataka wakaazi wa Tana Delta na kaunti nzima ya Tana River kudumisha amani wakati huu wa kampeni hata wakati wa uchaguzi akisema kuwa siasa ni za msimu hivyo basi watu wanapswa kuchunga maisha yao.