Maafisa wa polisi wanaosimamia mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE unaoendelea katika Kaunti ya Mombasa wametakiwa kumakinika mno na kutoruhusu wizi wa mtihani huo.

Mshirikishi mkuu wa utawala Kanda ya Pwani John Elungata amewatakamaafisa hao kuwajibika katika kuhakikisha hakuna visa vyovyote vya wizi wa mtihani vinavyoshuhudiwa katika vituo vya mtihani.

Akizungumza katika Gatuzi dogo la Jomvu hii leo aliposhuhudia usambazaji wa mtihani, Elungata amesema Maafisa hao watachukuliwa hatua za kisheria endapo watashirikiana na watu wengine katika kuiba mtihani.

Elungata ambaye alikuwa ameandamana na Kamanda mkuu wa polisi Pwani Manase Musyoka, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Lucas Mwanza pamoja na Mkurugenzi mkuu wa elimu Kaunti ya Mombasa Peter Magiri amesema juma hili halijakumbwa na kisa chochote cha utata na kwamba mtihani huo unaendelea vyema.

Mwandishi:Ibrahim Juma


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo