Wanaharakati wa kijamii katika kaunti ya Mombasa wamewalaumu viongozi wa kisiasa kwa madai ya kwamba wameshindwa kudhibiti ulanguzi na utumizi wa dawa za kulevya.

Wakiongozwa na Martha Wanza wa shirika la Young Women Christian Association amesema viongozi hao sasa wako kwenye harakati za kujitafutia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu huku swala hilo ambalo limekuwa kero kwa wakaazi wakilifumbia macho.

Amesema kuwa utumizi wa dawa za kulevya kwa sasa umekithiri hadi shuleni akiwalaumu viongozi kwa kutolikemea jambo hilo hadharani.

Kwa upande wake mwanaharakati wa maswala ya vijana kutoka kwa kamati ya amani ya eneo bunge la Nyali Christine Khabuya amewashutumu wanasiasa kwa kile anachokidai kuwa wananunua mihadarati na kuwapa vijana na kina mama ili kuzua vurugu hatua anayoitaja kuchangia uongozi duni wa kaunti hiyo.

Kauli zao zimeungwa mkono na naibu mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Nyali Ibrahim Menza na kusema kuwa swala la kukomesha matumizi ya mihadarati ni jukumu la kila mmoja katika jamii na wala sio wanaharakati pekee.

 


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani