Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba sio lazima nchi hiyo ipeleke wanajeshi wake nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kulingana na mkataba wa viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Kagame amesema kwamba matatizo ya usalama nchini Congo yanaletwa na serikali ya Congo yenyewe na kwamba vita haviwezi kumaliza shida iliyo mashariki mwa Congo.

Kagame ana Imani kwamba mzozo wa kiusalama unaondelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unapaswa kutatuliwa kwa njia za kisiasa badala ya matumizi ya nguvu.

Kagame alikuwa akizungumza mjini Kigali wakati Rwanda ikiadhimisha miaka 28 ya vita vya ukombozi wa nchi hiyo.

Nchi za jumuiya afrika mashariki zimekubaliana kutuma kikosi cha wanajeshi kwa ajili ya usalama mashariki mwa Jamhiri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo wanajeshi wa serikali wanaendelea kukabiliana na waasi wa kundi la M23.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imedai kwamba serikali yar ais wa Rwanda Paul Kagame, inahusika kwenye mzozo huo, kwa kuunga mkono na kuwasaidia waasi wa M23.

Rwanda imeanausha madai hayo na badala yake kudai kwamba DRC inaunga mkono waasi wa FDLR wanaotaka kuangusha utawala wa Kagame.

 Hisani ya VOA Swahili