Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi amewasili mjini Kuala Lumpur leo Jumanne, mji huo ukiwa kituo chake cha pili katika ziara ya barani Asia ambayo imezua ghadhabu nchini China juu ya uwezekano wa kukitembelea kisiwa cha Taiwan.

Shirika la habari la serikali la Bernama limeripoti kuwa Pelosi alitua katika kambi ya jeshi la anga la Malaysia, na anatarajiwa kufanya mkutano na Waziri Mkuu na spika wa bunge la nchi hiyo.

Baada ya Singapore na Malaysia, spika huyo wa bunge la Marekani anatarajiwa kuzitembelea Korea Kusini na Japan - japo uwezekano wa kuizuru Taiwan ndio kumesababisha tumbo joto.

Licha ya utawala wa Rais Joe Biden kuonekana kupinga safari hiyo ya Taiwan, msemaji wa Pentagon John Kirby amesema Pelosi ana haki ya kufanya ziara kokote anakotaka.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani