Meli ya kwanza iliyobeba shehena ya ngano kutoka Ukraine imewasili kwenye lango la bandari ya Bosphorus nchini Uturuki kwa ajili ya ukaguzi. Meli hiyo iliyoondoka bandari ya Odesa siku ya Jumatatu inadhamiria kutia nanga nchini Lebanon.

Hii ni shehena ya kwanza tangu Urusi kuzizuwia bandari za Ukraine kwenye Bahari Nyeusi baada ya kuivamia Ukraine mwezi Februari. Pande hizo mbili zilisaini makubaliano ya kuachia ngano ya Ukraine kusafirishwa, huku kukiwa na tatizo kubwa la ukosefu wa chakula ulimwenguni.

Shehena hii ya awali ina tani 26,000 ya ngano. Meli hiyo yenye bendera ya Sierra Leone ilipaswa kuchukuwa tahadhari ya juu wakati wa kupita kwenye bahari inayoaminika kutegeshwa mabomu mengi majini.

Misafara mingine ya meli inatazamiwa kufuatia siku chache zijazo. Kuzuiwa kwa bidhaa za Ukraine kumesababisha uhaba wa chakula na mfumuko mkubwa wa bei kote duniani.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani