Timu za Dumna na Black Eagle zimejiongezea matumaini ya kutinga katika hatua ya 16 bora baada ya kuwalaza wapinzani wao.

Katika mechi iliochezwa kwenye uga wa Denmark, Dumna imeendeleza makali yake kwenye michuano hiyo baada ya kuichabanga Uprising F.c kutoka Denyenye mabao 2-1.

Kwenye mechi yake ya kwanza katika kundi F, Dumna kutoka Vingujini Msambweni, waliipiga Timu ya kundutsi kutoka Tsimba mabao 3-1 katika mechi iliyogarazwa katika uwanja wa shule ya msingi ya mkokoni.

Kufikia sasa, Dumna inaongoza kundi F ikiwa na alama 6 huku ikiratibiwa kuvaana na Kinango United kwenye mechi yaop ya mwisho ya Kundi F.

Na katika uga wa shule ya upili ya Waa, Timu ya Black Eagles kutoka Dandora (Mbweka) ilijikatia tikiti ya mapema ya 16 bora baada ya kuilaza Kwale teachers mabao mawili kwa moja.

Timu hiyo ambayo haikuweza kushiriki msimu uliopita kwa kuwa ilikuwa imefungiwa kwa sababu ya ukosefu wa nidhamu wa Mashabiki wake, ilijipatia alama tatu za mezani baada ya wapinzani wao Wayzata kukosa kufika uwanjani.

Mechi yao ya mwisho ya makundi itakuwa ni dhidi ya Lazium kutoka kigato.

Kwenye mechi nyengine iliyogarazwa jana Marika ilitoka sare tasa na Lutembe kwenye ngarambe yao ya kundi E.