Kocha wa Coast Queens kutoka Kisauni inayocheza kwenye ligi ya FKF hapa Mombasa, Mohammed Mngaro ametoa wito kwa washikadau wa soka hapa Mombasa kujitokeza na kusaidia timu hiyo.

Akiongea baada ya mechi yao ya wikendi waliyoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ocean Starlet, kocha huyo amesema timu yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vifaa vya kuchezea pamoja na fedha za kusafiria ili kushiriki mechi zake za ugenini.

Kocha Mngaro ametoa wito kwa viongozi na jamii kujitokeza kusaidia ukuajiwa vipaji katika timu hiyo ya kinadada kutoka Kisauni.