Mechi za kukamilisha hatua ya makundi katika ligi ya Rashid Abdalla Super Cup zitapigwa wikendi hii ya 16 na 17 Septemba 2023 katika viwanja mbalimbali huko Kwale.

Siku ya jumamosi Zimbabwe watavaana na Azzam FC katika uwanja wa Denmark pale Maganyakulo.

Wasini united watoane kijasho na Kwale United kwenye uchanjaa wa Kombani.

Uwanjani Mkokoni kutashuhudiwa ngarambe kati ya Schalke 04 na Kombani Youth fc.

Bingwa mtetezi Denmark FC ambao wanapania kutetea ubingwa wao kwenye Makala haya ya nne watakuwa katika uga wa Waa kumenyana na Volacano.
Mechi zote za jumamosi zitaanza saa 3:30 alasiri.

Siku ya jumapili itakua zamu ya Dumna kumenyana na Kinango United katika uga wa Denmark.

Uprising wapepetane na Kundutsi uwanjani mkokoni.

Mshale FC watoane kijasho na Buster kwenye uga wa Waa.

Kitivo United watakapiga na Word of Life fc kwenye uchanjaa wa Kombani.

Mechi hizo za jumapili pia zitaanza saa 3:30 alasiri.